Vitambulisho vya Taifa ni chachu ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
- Vitasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali
- Vitasaidia kumtambua mhusika anapohitaji kupatiwa huduma katika taasisi mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya.
- Vitasaidia kumtambua mhusika anapohitaji kupatiwa huduma katika taasisi mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya.
- Vitarahisisha kuwatambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka kwenye benki na asasi mbalimbali za fedha nchini.
- Vitasaidia kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari la kumbukumbu la kielektroniki.
- Vitawezesha kumtambua mtu anapofanya biashara au shughuli nyengine kwa kutumia majina tofauti.
- Vitafanikisha kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii. Kwa mfano, kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo raia wa Tanzania anastahili.
- Vitasaidia kusaidia kuondoa watumishi hewa kwenye mfumo wa mishahara ya ‘payroll’ ya Serikali.
- Vitaimarisha utendaji kazi Serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za watumishi na malipo ya stahili zao, hasa pale wanapostahafu.
- Vitarahisisha zoezi la kuhesabu watu (sensa).
- Vitarahisisha zoezi la kuhuisha daftari la wapiga kura.
No comments:
Post a Comment